Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, kinagawa zaidi ya sahani (148,000) za chakula kila wiki.
Kiongozi wa idara ya chakula Hassan Muhammad Hashim amesema kuwa “Mgahawa unapika na kugawa zaidi ya sahani (10,000) katika siku za kawaida kuanzia Jumapili hadi Jumatano, siku ya Alkhamisi, Ijumaa na Jumamosi ambazo huwa na mazuwaru wengi, mgahawa hupika na kugawa zaidi ya sahani (36000) kwa siku”.
Akaongeza kuwa “Chakula cha mchana na usiku hutolewa kila siku, kazi ya kugawa chakula kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) inafanywa muda wote”.
Kiongozi wa idara ya chakula akasema kuwa “Asilimia kubwa ya chakula kinachopigwa kinatoka kwenye shirika la Nurul-Kafeel, tunawapishi hodari na mahiri”.