Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefungua semina ya Qur’ani katika mkoa wa Dhiqaar.
Mkuu wa tawi la Maahadi hiyo bibi Maha Abbasi amesema “Maahadi imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanawake na wasichana, tumefanikiwa kufanya semina (13) za Qur’ani kwenye vitongoji tofauti vya mkoa wa Dhiqaar”.
Akaongeza kuwa “Semina zimejikita katika kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani pamoja na kuhifadhi, semina za kuhifadhi zipo (8) na semina za usomaji kwa kuzingatia kanuni za tajwidi zipo (5), zimehusisha wasichana wenye umri tofauti”.

