Pamoja na mwenzake katika Atabatu Husseiniyya.. Kituo cha utamaduni wa familia kinajadili njia za kusaidiana na kushirikiana

Ugeni wa kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya umetembelea kituo cha mwongozo wa familia katika Atabatu Husseiniyya na kujadili njia za kusaidiana na kushirikiana baina yao.

Mkuu wa kituo cha utamaduni wa familia bibi Sara Hafaar amesema “Ziara hii ni sehemu ya kujenga ushirikiano baina yetu, na kutoa huduma bora katika jamii na familia za watu wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Ugeni umeeleza harakati zake na mipango yao ya baadae, sambamba na kueleza huduma mbalimbali wanazotoa katika kutengeneza familia zenye maadili mazuri zinazofuata misingi ya Dini ya kiislamu na mwenendo wa Ahlulbait -a.s-”.

Naye kiongozi wa Maahadi ya familia za kiislamu bibi Rafaa Hakim amepongeza ziara hii, akasema kuwa ni njia nzuri ya kujenga ushirikiano baina yao, na kubadilishana uzowefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: