Marekani.. Atabatu Abbasiyya inashiriki katika kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s)

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika bara la Amerika kaskazini na kusini, ameshiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s) yaliyofanyika nchini Marekani.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya nchini Marekani Shekhe Muhammad Jawadi Salami amesema “Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetokana na mwaliko tuliopata kutoka kwa jamii ya waislamu wenye asili ya India waishio Marekani, katika hafla hiyo tumezungumza kuhusu ushujaa na Subira ya bibi Zainabu (a.s) na uhusiano wake na Imamu Abbasi (a.s) kwa mujibu wa maelezo ya Shekhe Salami”.

Baada ya hapo ikafanywa hafla ya kufungua bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wahudhuriaji wakatabaruku kwa bendera hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: