Katika shindano la Qur’ani la kitaifa.. Majmaa-Ilmi imetoa mshindi wa kwanza

Msomaji wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya amekua mshindi wa kwanza kwenye shindano la Qur’ani la kitaifa awamu ya nane.

Majmaa imewakilishwa na msomaji wa Maahadi ya Qur’ani bwana Ali Zubaidi, aliyepata nafasi ya kwanza kwenye shindano la Qur’ani la kitaifa awamu ya nane, linalo husisha vyuo vikuu vya Iraq, shindano lilikua la kuhifadhi na kusoma, chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Masjidi Kufa.

Washiriki wa shindano hilo wametoka kwenye vyuo vikuu zaidi ya thelathini mikoa tofauti ya Iraq, na yamedumu kwa muda wa wiki mbili.

Zubaidi amesifu kazi inayofanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu, ya kuwajengea uwezo wa kuhifadhi na kusoma Qur’ani jambo ambalo limepelekea kupata ushindi huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: