Katika mkoa wa Muthanna.. Majmaa-Ilmi inaendelea na mahfali za mimbari za nuru ya Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea kufanya mahfali za usomaji wa Qur’ani kupitia mradi wa (Mimbari za nuru) kila wiki.

Mradi huo unasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Mkuu wa kituo Sayyid Hassanaini Halo amesema “Kituo cha miradi ya Qur’ani kimefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani (mimbari za nuru) katika mkoa wa Muthanna, kwa kushirikiana na umoja wa wasoma Qur’ani wa mkoa huo”, akabainisha kuwa “Usomaji huo wa Qur’ani umefanywa ndani ya Husseiniyya ya Answaru Zaharaa (a.s)”.

Akaongeza kuwa “wasomaji walikua ni Sayyid Muhammad Ridhaa Zubaidi, wasomaji wawili kutoka mradi wa kiongozi wa wasomaji ambao ni, Sayyid Sajjaad Hussein na Sayyid Hussein Ali, huku muongozaji wa hafla akiwa ni Sayyid Hassanaini Jazaairiy”.

Hafla imehudhuriwa na watu wengi miongoni mwa waumini wanaoushi Jirani na Husseiniyya hiyo, Pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za Qur’ani za mkoani hapo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: