Mjumbe wa kamati kuu amesema: Miradi ya Atabatu Abbasiyya inalenga kujenga mustakbali wa mwanaadamu na kulinda haki zake

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya inalenga kujenga mustakbali mwema wa mwanaadamu na kulinda haki zake.

Katika ujumbe aliotoa kwa vyombo vya Habari amesema kuwa, miradi hiyo inalinda haki za binaadamu bila kuathiri haki za watu wengine.

Akaongeza kuwa: hapa nazungumzia mkakati wa kimataifa wa (malengo endelevu), toka yalipotangazwa mwaka 2015 Atabatu Abbasiyya imesha tekeleza malengo mengi kupitia miradi mbalimbali tunayofanya.

Akaendelea kusema, ukiangalia upande wa afya utakuta Atabatu Abbasiyya iko mstari wa mbele katika kutekeleza hilo, hali kadhalika katika sekta ya elimu na mambo mengine, hakika Atabatu Abbasiyya iko mstari wa mbele katika kila nyanja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: