Kazi ya kuweka kitambaa kipya kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) imekamilika.
Shughuli za kuweka kitambaa kipya zimehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, rais wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Shimri, katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo, mkuu wa mkoa wa Karbala na kundi la waumini.
Yamefanywa maandalizi makubwa ya kuweka kitambaa kipya kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kukamilika kazi kubwa ya kutengeneza kitambaa hicho, iliyochukua miaka mitatu na kuhusisha mataifa ya Misri, Siriya, Ufaransa na Kuwait.
Kitambaa kipya kimepambwa na nguzo (16) za dhahabu zilizo andikwa majina ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kila upande unanguzo nne, hali kadhalika kila upande unapicha ya kiganja za Abbasi (a.s) iliyopambwa kwa dhahabu na lulu, majina matukufu yamenakshiwa kwa Duru-Najafu ambayo imepamba kitambaa upande wa kichwa na miguu.
Aina ya uwekwaji wa dhahabu na fedha iliyotumika kwenye kitambaa hiki inatofautiana na vitambaa vya zamani, upande wa umadhubuti na kiwango cha dhahabu kilicho tumika, hii ni aina mpya kitaalamu, ikumbukwe kuwa kitambaa hiki kimefadhiliwa na kamati ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka Kuwait yenye ubobezi na uzowefu mkubwa wa kutengeneza vitambaa vya kufunika kwenye makaburi matakatifu.
















