Shule za Al-Ameed zimepokea ugeni kutoka Nainawa na Waasit

Shule za Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya zimepokea ugeni kutoka chuo kikuu cha Mosul na taasisi ya bibi Zainabu (a.s) kutoka Waasit.

Ugeni huo umekuja kuangalia uzowefu wa shule za Al-Ameed katika sekta ya malezi na elimu ya juu, na kuangalia vifaa vya kisasa vinavyotumika kufundishia.

Ugeni huo umefurahishwa sana na majengo ya shule sambamba na ubora wa upangiliaji wa shule za awali, msingi na sekondari bila kusahau kumbi za michezo na vifaa vya kisasa vilivyopo kwenye kumbi hizo.

Mkufunzi wa chuo kikuu cha Mosul Dokta Rayaan Abbasi amesema “Shule za Al-Ameed zinampangilio mzuri na zinatoa elimu bora, sio kwa kiwango cha mkoa wa Karbala tu, baili kwa kiwango cha taifa zima la Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: