Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amemtembelea Mheshimiwa Shekhe Baaqir Maqdasi nyumbani kwake (katika mji wa Qum) nchini Iraq kumjulia hali.
Mheshimiwa katibu mkuu amefikisha dua na salam za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na kupongeza kazi kubwa aliyofanya ya kufundisha elimu na utamaduni wa Ahlulbait (a.s), sambamba na kuelezea mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s).
Katibu mkuu amekabidhi bendera tukufu kutoka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa Shekhe Maqdasi, aidha amemuahidi kumpa huduma za matibabu kwenye hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kuonyesha thamani ya kazi kubwa aliyofanya ya kuhudumia mimbari ya Imamu Husseini (a.s).



