Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Swidiqatu Twahirah (a.s)

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Swidiqatu Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Majlisi itaendelea kwa muda wa siku mbili nayo ni sehemu ya ratiba ya Ataba tukufu ya uombolezaji wa kifo cha mtoto wa Mtume bibi Zaharaa (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ukafuata mhadhara kutoka kwa Shekhe Qassim Hashimi aliyezungumza kuhusu bibi Zaharaa (a.s), ameeleza historia yake na nafasi yake mbele ya baba yake na Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Majlisi hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake, imehitimishwa kwa kusomwa tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi katika nyoyo za waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: