Majmaa-Ilmi imehitimisha semina ya usomaji bora

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha semina ya (usomaji bora).

Semina hiyo imesimamiwa na idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara Sayyid Ahmadi Zamili amesema “Semina ilianza mwezi wa kumi uliopita, na imedumu kwa muda wa miezi mitatu, kila wiki wamesoma siku mbili, wamefundishwa kanuni za usomaji wa Qur’ani chini ya usimamizi wa Dokta Karim Zubaidi”.

Washiriki wamefanya mitihani miwili, mtihani wa nadhariyya na mtihani wa vitendo, walikua zaidi ya washiriki thelathini.

Idara ya usomaji wa Qur’ani inajitahidi kuelimisha jamii usomaji sahihi wa Qur’ani katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: