Majmaa-Ilmi inafanya majlisi ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Furaatu-Ausat

Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Furaatu-Ausat katika mji wa Najafu.

Program hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Nayo ni katika mradi maalum wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi awamu ya tatu mwaka wa (2022 – 2023).

Kikao kilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Akbaru Zaadah, ukafuata mhadhara uliotolewa na Sayyid Ahmadi Mussawi kisha yakafuata maoni na maswali kutoka kwa wanafunzi.

Majlisi ikafungwa kwa kupiga kura za kutafuta washindi waliopewa zawadi kutoka katika baraka za malalo takatifu ya Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: