Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Uongozi mkuu wa chuo cha Alkafeel, umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na mhadhara kutoka kwa Mheshimiwa Sayyid Jafari Murawwij, ameeleza historia tukufu ya Ummul-Banina (a.s) na mambo muhimu yaliyotokea katika Maisha yake.

Viongozi wakubwa wa chuo na baadhi ya watumishi wameshiriki kwenye majlisi hiyo, wametoa rambirambi zao kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: