Kitengo cha uboreshaji kimeandaa warsha kuhusu utatuzi wa changamoto

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa warsha ya utatuzi wa changamoto kwa viongozi wa idara za Ataba tukufu.

Mkufuzi wa warsha hiyo Sayyid Muhammad Abdulhussein amesema “Warsha inalenga kuboresha utendaji wa watumishi wa Ataba, pamoja na usimamizi bora wa miradi”.

Akaongeza kuwa “Warsha ilikuwa na mada nyingi, miongoni mwa mada hiyo ni namna ya kubaini tatizo, kuchambua njia za utatuzi wa tatizo, uchambuzi wa mbinu za kimkakati na kiuchumi, kuandaa mpango kazi na kuweka mkakati wa utekelezaji”.

Warsha hiyo itadumu kwa muda wa siku mbili, inafanywa ndani ya ukumbi wa Naafidhul-Baswirah, kila siku wanasoma kwa muda wa saa tano, kwa mujibu wa maelezo ya Abdulhusseini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: