Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinaendesha program ya kitamaduni (Nuru juu ya nuru) kwa wanafunzi wa shule ya Fadak-Zaharaa (a.s) ya Qur’ani kwa wasichana.
Program imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ikawasilishwa mada isemayo (siri ya furaha ya kweli) na Adhraa Ahmadi, halafu zikaonyeshwa picha na kutolewa maelezo na mlinganiaji Alyaasiriy.
Program hiyo ilikua pia na kipengele cha (kutoka kwenu hadi kwenu) ambacho ni maswali na majibu kutoka kwa wanafunzi.
Program hiyo inalenga kujenga utamaduni wa maelewano na utulivu katika familia kwa mujibu wa mwenendo wa Ahlulbait (a.s).