Sayyid Swafi amekutana na ugeni kutoka jamhuri ya Boznia

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amekutana na ugeni kutoka jamhuri ya Boznia na Harsak katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Msimamizi wa ziara hiyo Sayyid Baaqir Yaasiriy amesema: “Tulipo kutana na Sayyid Swafi tulijihisi sawa na kukutana kwa baba na mwanae, kwa jinsi alivyo tujali na alivyo kua akiuliza hali za waislamu wa Boznia, hakika tumehisi amani na utulivu sawa na mtoto anapokua mbele ya baba yake”.

Bibi Amira Korena mmoja wa wageni hao amesema: “Hii ni ziara yangu ya kwanza kuja katika mji wa Karbala, hakika raia wa Iraq wanatabia za wafuasi wa Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Nimebahatika kukutana na Sayyid Swafi, huu ni utukufu mkubwa sana kwangu, hakika yeye ni mtu mkubwa katika jamii”.

Wageni wakaeleza hali ya amani, jamii, uchumi na siasa ya Boznia, wakaonyesha matumaini yao ya kuendelea kukutana katika matukio mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: