Katika mji wa Kirkuuk.. kitengo cha habari kimehitimisha semina ya kujenga uwezo wa wanahabari.

Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kimehitimisha semina ya kujenga uwezo iliyoandaliwa kwa kushirikiana na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi, kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana katika sekta ya habari mkoani Kirkuuk.

Mshiriki kutoka kituo cha Alkafeel Sayyid Hussein Yaasiri amesema “Semina hiyo imefanywa kwa ushirikiano na viongozi wa mji wa Bashiir chini ya kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (kikosi namba 26 Hashdu-Shaabi), ikiwa na washiriki ishirini kutoka kitongoji cha Taazah na Bashiir katika mkoa wa Kirkuuk”.

Akaongeza kuwa “Wanasemina wamefundishwa mambo muhimu kuhusu upigaji wa picha kwa kutumia kamera za kisasa na kamera maalumu za simuganja za kisasa, pamoja na uhandisi wa picha, wakufunzi wa semina hiyo ni Haidari Jaliil, Abbasi Asadi, Muntiir Hassan Alkhatwiib na mhandisi wa sauti Mustwafa Imaad”.

Kwa mujibu wa Yaasir, hatua hii ni sehemu ya kujenga utu baada ya vita, kwa lengo la kujenga uwezo wa waandishi wa habari wa miji hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: