Majmaa-Ilmi imekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho ya kimataifa ya msahafu mtukufu

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye awamu ya pili ya maonyesho ya kimataifa ya msahafu mtukufu.

Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema “Ziara yetu ya ufatiliaji imeangalia maandalizi ya mwisho kufanywa na Majmaa, kuelekea ushiriki wa maonyesho ya kimataifa ya msahafu mtukufu yanayo simamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Ushiriki wa Majmaa utakuwa wa aina yake, unaoendana na hadhi ya Ataba tukufu, kwani imekuwa ikifanya vizuri kwenye sekta ya Qur’ani tangu mwaka (2014) kupitia chapisho lake la Qur’ani tukufu”.

Akabainisha kuwa “Maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho hayo yanafanywa kwa kiwango cha juu, kuna mbinu mpya katika sekta za Qur’ani hususan upande wa uchapishaji, zitaonekana siku zijazo”.

Mkuu wa kituo cha uchapishaji wa misahafu Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema “Katika maonyesho haya tumeongeza baadhi ya vitu, kutokana na mtazamo mpya wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inayojikita katika kuhudumia vizito viwili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: