Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba maalum kwa vijana wa wilaya ya Madina katika mkoa wa Basra.
Ratiba hiyo inasimamiwa na kituo cha Multagal-Qamar chini ya kitengo.
Ratiba inamihadhara miwili, wa kwanza umetolewa na Shekhe Mustafa Idani, ametambulisha harakati za kituo na huduma wanazotoa kwa vijana.
Huku mhadhara wa pili ukieleza (hatari na changamoto za sasa na utatuzi wake), umetolewa na mtafiti Sayyid Muhammad Hassan mbele ya washiriki (75) kutoka maeneo tofauti ya wiliya.