Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, umepongeza idara ya malezi ya mkoa wa Karbala katika siku ya mwalimu.
Pongezi zimetolewa baada ya ugeni huo kutembelea ofisi za idara ya malezi.
Mkuu wa idara ya malezi ya Karbala Sayyid Abbasi Auda amesema “Tunashukuru Atabatu Abbasiyya na kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi kwa kutukumbuka na kuja kututembelea katika siku hii adhim, hakika ziara hii inaonyesha wazi jinsi wanavyojali sekta ya malezi na elimu”.
Akaongeza kuwa “Ziara hii inatupa moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa bidi na kuinua kiwango cha elimu hapa nchini”.
Kila mwaka wakati wa sikukuu hii tarehe moja mwezi wa pili, Atabatu Abbasiyya hutuma salamu za pongezi kwa watumishi wote wa sekta ya elimu, kutokana na jukumu kubwa walilo nalo la kuwasha taa la elimu na maarifa.