Kiongozi wa hospitali ya Jabalah katika mkoa wa Laadhiqiyya nchini Sirya Dokta Muhammad Quswai, amepongeza kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya ya kusaidia hospitali hiyo kwa kuipa vifaa-tiba.
Amesema kuwa “Hakika Atabatu Abbasiyya imetoa msaada mkubwa sana kwa waathirika wa tetemeko nchini Sirya”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imetoa kiwango kikubwa cha dawa na vifaa-tiba” akasisitiza kuwa “Kupitia misaada hiyo tumeweza kutibu wagonjwa wengi”.
Dokta Quswai ametoa shukrani za dhati kwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusaidia hospitali za Iraq na waathirika wa tetemeko la ardhi.
