Chuo cha Malkia wa Wingereza kimechagua hospitali ya Alkafeel kuwa mahala pakufanyia mitihani ya udaktari kwa wanafunzi wake.

Idara ya hospitali ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuwa chuo cha Malkia wa Wingereza kimechagua hispitali hiyo kuwa mahala pakufanyia mitihani ya udaktari kwa wanafunzi wake.

Kiongozi wa hospitali hiyo Dokta Jaasim Saidi Ibrahimi amesema kuwa “Hospitali inajiandaa kuwapa mitihani wanafunzi wa udaktari kutoka chuo cha Malkia wa Wingereza, mitihani hiyo itatolewa na kusimamiwa na madaktari bingwa wa kiiraq wanaofanya kazi kwenye hospitali hiyo”.

Akaongeza kuwa “Watapewa mitihani ya (SCE) na sehemu ya pili “PACES” itahusu upimaji wa kitanda”. Akabainisha kuwa “Chuo cha Malkia wa Wingereza kimechagua hospitali hii kuwa mahala pakufanyia mitihani wanafunzi wake baada ya kuridhika na uwezo wa hospitali na vifaa-tiba vya kisasa ilivyonavyo”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ibrahimi, kawaida mitihani hiyo hufanywa nje ya Iraq na maranyingi katika nchi ya Wingereza, baada ya hospitali ya Alkafeel kukamilisha mahitaji yote ya lazima kwa ajili ya mitihani hiyo, imechaguliwa na chuo cha Malkia kuwa mahala pakufanyia mitihani kwa wanafunzi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: