Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Muhammad Harbi amesema kuwa “Wahudumu wa kitengo chetu wanatoa huduma za lazima kwa mazuwaru ndani ya mwezi wa Ramadhani, wanagawa maji baridi ya kunywa wakati wa futari, wametandika maeneo yote yanayo zunguka Ataba tukufu kwa ajili ya kupumzika mazuwaru na kufturu sambamba na kutandika eneo la uwanja wa mlango wa Kibla hadi kwenye uwanja mkuu”.
Akaongeza kuwa “Baada ya futari wanasafisha maeneo yote yaliyotandikwa, ngazi, vyoo, kwa kutumia watu na mitambo ya usafi”.
Akaendelea kusema “Tunaweka mazingira mazuri ya kufuturu kwa mazuwaru wanaokuja kutoka mikoa tofauti ya Iraq, sambamba na kuandaa mazingira bora ya kiroho”.