Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s).

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s).

Majlisi inafanywa baada ya swala ya Alfajiri kwa muda wa siku tatu mfululizo kwenye uwanja huo.

Majlisi imepata mahudhurio makubwa kutoka kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shekhe Muhammad Rikabi katika siku ya kwanza ameongea kuhusu kifo cha Imamu Ali (a.s) na historia yake katika Dini ya kiislamu.

Naye muimbaji Aali-Twaama akasoma kaswida zilizo eleza tukio la kuhuzunisha nyoyo za waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: