Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya semina ya kiitikadi kuhusu kumtambua Mwenyezi Mungu katika nchi ya Naijeria barani Afrika.
Semina hiyo imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Semina iliyofanywa inahusu kumtambua Mwenyezi Mungu na tauhidi ya kweli, sambamba na kujibu fikra batili zinazopotosha tauhidi iliyofundishwa na Mtume mtukufu”.
Akasema kuwa “Lengo la semina ni kuwajengea uwezo waislamu wa Afrika, wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Semina imefanywa baada ya kuwasiliana na mubalighi wa Markazi katika mji wa Kaduna nchini Naijeria Shekhe Amiin Abu Bakari Swadiq, na kuhudhuriwa na wafuasi wengi wa Ahlulbait (a.s)”.