Ugeni wa kitengo cha habari na utamaduni umehudhuria kwenye kongamano la balozi awamu ya kumi na mbili.

Ugeni kutoka kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, umehudhuria kwenye kongamano la balozi awamu ya kumi na mbili linalo simamiwa na uongozi mkuu wa Masjidi Kufa na mazaru zilizochini yake.

Rais wa ugeni huo na muwakilishi wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Sayyid Muslim Aljabiri amesema, hakika kuhudhuria kwetu hapa ni sehemu ya kujenga ushirikiano kati ya Ataba na mazaru tukufu na kuwa daraja la ushirikiano katika harakati za kielimu na kitamaduni.

Akafafanua kuwa, mubalighina wa kiafrika kutoka Markazi na wanafunzi wa Dini wameshiriki katika ugeni huu.

Kongamano hili ni kumbukizi ya kuwasili mjumbe wa Imamu Hussein (a.s) Muslim bun Aqiil (a.s) katika mji wa Kufa, kwa mujibu wa maelezo ya Aljaabiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: