Majmaa-Ilmi imefanya kikao cha kujadili mradi wa semina za kiangazi katika jiji la Bagdad.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mkutano wa maandalizi ya semina za Qur’ani wakati wa majira ya kiangazi katika jiji la Bagdad.

Mkutano huo umefanywa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad chini ya Majmaa, wamejadili hatua za mwisho katika maandalizi ya semina za majira ya kiangazi zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Washiriki wamejadili namna ya kurahisisha usajili wa wanafunzi na kugawa majukumu ya walimu kutokana na vitongoji, kitongoji cha Karkha, Raswafa, na sehemu zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: