Katika mji wa Diwaniyya.. Majmaa-Ilmi inafanya warsha ya kujenga uwezo kwa walimu wa semina za Qur’ani.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya warsha ya kuwajengea uwezo walimu wa Qur’ani katika mkoa wa Diwaniyya.

Warsha hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu.

Muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu katika mkoa huo Shekhe Baasim Waaili ameshiriki kwenye warsha hiyo pamoja na mtafiti na muandishi wa mambo ya kijamii Ustadh Haidari Muhammad Kaabi, bila kusahau kiongozi wa idara ya harakati za Qur’ani katika Maahadi Sayyid Zaidi Rimahi, ametaja kwa urefu ratiba ya mradi huo.

Warsha inalenga kukuza uwezo wa walimu na kuwaelekeza njia za ufundishaji za kisasa unaotumika katika mradi wa Qur’ani wa majira ya kiangazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: