Ugeni wa kamati ya malezi kutoka mkoa wa Baabil umepongeza njia za kisasa zinazotumika kufundishia katika shule za Al-Ameed.
Hayo yamesemwa wakati wageni hao walipotembelea maeneo muhimu ya shule hizo, na kuangalia kumbi za madarasa, vifaa vya kufundishia pamoja na kuongea na walimu.
Katika ziara hiyo wameangalia majengo ya shule za (msingi na sekondari), bila kusahau shule za awali (chekechea) na kumbi za michezo.
Ugeni ukapongeza njia za kisasa zinazotumika katika ufundishaji na mchango mkubwa unaotolewa na shule hizo katika sekta ya malezi na elimu hapa nchini.