Idara ya wahadhiri tawi la wanawake inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Aljawaadi (a.s).

Idara ya wahadhiri tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Taghrida Tamimi amesema “Idara imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaadi (a.s), ikasomwa ziara maalum ya Imamu Aljawaadi (a.s) ikafuatiwa na mhadhara ulioeleza historia tukufu ya Imamu na maeneo muhimu katika Maisha yake”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imehitimishwa kwa kusoma qaswida za kuomboleza na Duau-Faraj”, akabainisha “Nafasi ya shia katika kufanya majlisi za kuomboleza kumbukumbu za vifo vya Ahlulbait (a.s) katika maeneo tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: