Tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya limeadhimisha kumbukizi ya ndoa ya Nuru kwa Nuru (Ali na Fatuma -a.s-).
Hafla imefanywa katika matawi ya Maahadi kwenye kitongoji cha Ifaar mkoani Baabil na wilaya ya Hindiyya mkoani Karbala.
Mkuu wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema, Hakika hafla hizo zimefafanua matukio muhimu ya mwezi wa Dhulhijjah, pamoja na kupambwa kwa Qur’ani, tenzi za kidini na maigizo kuhusu utukufu wa kiongozi wa waumini na Fatuma Zaharaa (a.s).
Kwa mujibu wa maelezo ya Aljaburi, kutoka kwa kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo “Wafuasi wetu wameumbwa kutokana na udongo wetu na wamechanganywa kwa maji ya uongozi wetu, wanahuzunika kwa huzuni zetu na wanafurahi kwa furaha zetu”, aidha maadhimisho haya ni sehemu ya kujenga utamaduni wa kuwapenda Ahlulbait (a.s).
Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake akasisitiza kuwa “Maahadi hutilia umuhimu mkubwa kuadhimisha matukio kama haya na kuendesha semina za majira ya kiangazi kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani na kuimarisha misingi ya kiislamu”.