Maahadi ya turathi za mitume (a.s) idara ya wanawake, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya inawatahini mubalighina watakaoshiriki kwenye ziara ya Arubaini.
Mitihani imetolewa kwa kushirikiana na mradi wa Dini katika mji wa Najafu, watahiniwa ni mubalighina kutoka sehemu tofauti za Iraq.
Mitihani hiyo ni sehemu ya kuandaa mubalighina watakao shiriki kutoa elimu ya Dini wakati wa ziara ya Arubaini, inafanywa ndani ya ukumbi wa Shekhe Answari katika mji wa Najafu, majibu yatatolewa hivi karibuni baada ya kamati ya majaji kukamilisha kazi yake.
Mugalighina wa kike watasambazwa sehemu mbalimbali za Barabara zote zinazoelekea Karbala, wakati wa ziara ya Arubaini.