Mawakibu za watu wa Baabil zimeomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika uwanja wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Kiongozi wa mawakibu za watu wa Baabil Sayyid Swalahu Haadi amesema “Watu wa Baabil wamezowea kuja Karbala kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika siku ya kumbukumbu ya kifo chake kupitia mawakibu zao na kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Akaongeza kuwa “Maukibu ya pamoja imefanywa chini ya bendera ya maombolezo ya watu wa Baabil baada ya swala ya Adhuhuri, jambo hilo limefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya”.
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, huteua watumishi wake ambao hufuatana na maukibu kuanzia mwanzo hadi mwisho, wanajukumu la kusimamia matembezi na kuhakikisha hakutokei msongamano wowote wala usumbufu kwa mazuwaru.