Majmaa-Ilmi inafunga semina ya maandishi ya msahafu kwa kutoa mtihani wa mwisho kwa wanafunzi.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha semina ya (Maandishi ya Qur’ani) kwa kuwapa mtihani washiriki.

Semina imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Mtihani unalenga kutambua kiwango cha mwanafunzi na namna alivyonufaika na masomo aliyofundishwa kwa kipindi cha miezi miwili, kila wiki walipata mihadhara miwili, jumla ya washiriki walikuwa (30)”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi wamesoma mada tofauti, ikiwemo ya maandishi ya msahafu na historia yake, pamoja na nadhariya za uandishi wake, chini ya mkufunzi Dokta Karim Zubaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: