Kitengo cha habari na utamaduni kumefungua kisima kipya katika nchi ya Chadi.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefungua kisima kipya katika nchi ya Chadi kupitia mradi wake wa Saaqi Atwasha Karbalai kwenye bara la Afrika, ufunguzi wa kisima umesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Kisima kipya kimefunguliwa katika nchi ya Chadi mbele ya muwakilishi wa Markazi Shekhe Ali Muhammad na kundi la wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Ataba inaendelea kufanya miradi ya kibinaadamu katika bara la Afrika sambamba na kuendesha program za kielimu ambazo huendeshwa na wawakilishi wake waliope kwenye nchi tofauti za Afrika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: