Njia ya kuelekea peponi.. matembezi ya Arubaini yameingia kwenye wilaya ya pili ya mkoa wa Dhiqaar.

Matembezi ya mazuwaru wa Arubaini wanaokwenda Karbala yameingia kwenye wilaya ya pili ya mkoa wa Dhiqaar.

Ripota wetu anasema “Mazuwaru wamefika kwenye wilaya ya Fuhuud mashariki ya mkoa wa Dhiqaar umbali wa (km 310) kutoka kitongoji cha Raasu Shaibah, sasa hivi wapo kwenye wilaya ya Jabaishi ambayo ni kituo cha kwanza katika mkoa wa Dhiqaar, wanatarajiwa kutembea (km 365) hadi kufika Karbala”.

Akaongeza kuwa “Mawakibu Husseiniyya zilizopo katika wilaya hiyo zinatoa huduma tofauti kwa mazuwaru ikiwa ni pamoja na kuandaa sehemu za kupumzika, huku wakazi wakifungua milango ya nyumba zao na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru”.

Mkoa wa Dhiqaar ndio mji wa pili kufikiwa na mazuwaru wanaotoka Basra kusini mwa Iraq, baada ya mikoa hii miwili wataungana wakazi wa mikoa ya kusini na mikoa ya kati kwenye matembezi hayo ya kukumbuka arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: