Idara ya wahadhiri tawi la wanawake inahuisha kifo cha Imamu Hassan (a.s) kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imehuisha kifo cha Imamu Hassan (a.s) kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza.

Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi amesema “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na historia ya Imamu Hassan (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na igizo lenye anuani isemayo (Koo yenye sumu), limeonyesha sababu za Imamu Almujtaba (a.s) kukubali sulhu na Muawiya na mpango wa kutekwa kwake”.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za kuomboleza pamoja na Dua ya Faraj na kutoa rambirambi kwa Imamu wa zama (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: