Anaangalia maandalizi ya ziara ya Arubaini.. Sayyid Swafi anafanya ziara katika jengo la Abulfadhil Abbai (a.s) linalotumika kuhudumia mazuwaru.

Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ametembelea jengo la Abulfadhil Abbasi (a.s) linalotumika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini na kukagua maandalizi ya mwisho.

Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea jengo la Abulfadhil Abbasi (a.s) lililopo Barabara ya (Najafu – Karbala) akiwa na katibu mkuu wa Ataba tukufu, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na watumishi wa kitengo cha miradi.

Mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu na kiongozi wa jengo hilo Sayyid Jawaad Hasanawi amesema “Ziara ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika jengo la Abulfadhil Abbasi (a.s), ni kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini watakaokuja kutoka ndani na nje ya nchi”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa Ataba wamekamilisha maandalizi hivi karibuni, wamefanya upanuzi wa jengo na kuongeza maeneo mapya ya kutoa huduma kwa idadi kubwa ya mazuwaru”.

Jengo linatarajia kutoa kuduma kwa mazuwaru siku chache zijazo, jengo linasehemu mbili, ya wanaume na wanawake, linakila kitu kinachohitajiwa na zaairu, kuna eneo la vyoo na sehemu ya kutolea huduma za matibabu.

Eneo la jengo linaukubwa wa dunam (15), kuna ukumbi wenye ukubwa wa mita 15000, eneo la kituo cha afya linaukubwa wa mita 600 na eneo la vyoo linaukubwa wa mita 2000.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote, imeweka mkakati maalum kwa kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: