Kitengo cha Dini kinafanya kazi kubwa ya Tablighi kwa mazuwaru wa Arubaini.

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa huduma ya Tablighi katika jengo la Shekhe Kuleini lililopo Barabara ya (Baghdad – Karbala).

Shekhe Qassim amesema kuwa “Jengo la Shekhe Kuleini linapokea maelfu ya watu kila siku wanaokuja kuuliza maswali ya kifiqhi, kimaadili, kiaqida na kijamii, wahudumu wetu huwapa majibu na ufafanuzi wa kisheria”.

Akaongeza kuwa “Wahadhiri wanatoa nasaha na muongozo, wanafikisha maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kwa mazuwaru wanaokuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.

Kitengo cha Dini hufungua vituo vya kujibu maswali kisheria na kutoa maelekezo ya kidini kwa mazuwaru wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: