Muandishi wa habari kutoka Uturuki amesema: Atabatu Abbasiyya imerahisisha urushaji wa matukio ya ziara ya Arubaini.

Muandishi wa Habari kutoka nchini Uturuki bwana Aghuri Akashi amesema kuwa Atabatu Abbasiyya imerahisisha jukumu la urushaji wa Habari zinazohusiana na ziara ya Arubaini.

Atabatu Abbasiyya ilifungua kituo maalum kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa Habari kwa wanahabari waliokuja Karbala kutoka ndani na nje ya Iraq.

Akashi ambae ni mkuu wa chanel 14 nchini Uturuki akasema “Atabatu Abbasiyya kupitia kituo chake cha Habari za ziara ya Arubaini, imerahisisha sana upatikanaji wa Habari za ziara ya Arubaini kwenye mazingira yenye msongamano kubwa wa mamilioni ya watu”.

Akaongeza kuwa “Kituo kilitupa vifaa vya kufanyia kazi tulivyo hitaji, sambamba na kuandaa sehemu maalum za kufanyia mahojiano ya kwenye televisheni (luninga), mbapo tumepata picha nzuri na sauti tulivu na tumefanikiwa kuufikishia ulimwengu matukio halisi ya ziara ya Arubaini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: