Kitengo cha maarifa kinaomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Basra.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kinaomboleza kifo cha mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza katika mkoa wa Basra.

Majlis hiyo imesimamiwa na kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo.

Mzungumzaji alikuwa ni Dokta Murtadha Maduhu, ameongea kuhusu tukio la kifo cha Mtume (s.a.w.w) na sifa zake sambamba na kueleza historia na jitihada kubwa aliyofanya (s.a.w.w) katika kufikisha ujumbe wa Dini tukufu ya kiislamu hadi roho yake takatifu ilipotoka na Kwenda kwa Mola wake mtukufu.

Majlisi imefanywa ndani ya ofisi za kituo katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi kutokana na kumbukizi ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: