Wizara ya elimu ya juu imetoa zawadi kwa rais wa chuo kikuu cha Alkafeel wakati wa ushiriki wake kwenye maonyesho na kongamano la kielimu la Iraq.

Waziri wa elimu ya juu na tafiti za kielmu Dokta Naim Abudi, amemkabidhi zawadi mkuu wa chuo cha Alkafeel Dokta Nuris Dahani, alipohudhuria maonyesho na kongamano la kielimu jijini Baghdad.

Dahani ameshiriki kikao kilichofanywa pembezoni kwa kongamano chini ya usimamizi wa muwakilishi wa wizara kwenye sekta ya tafiti za kielimu Dokta Haidari Abdu Dhwahadi.

Mwenyekiti wa kikao hicho amekubali ushirikiano na amesaini msaada wa utoaji wa mali baina ya chuo cha Alkafeel na wizara, unahusisha ukusanyaji wa mali kutoka kwenye vyuo vikuu vya serikali na binafsi, hivyo kutakuwa na ushirikiano wa kimali baina ya taasisi za kielimu na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Muwakilishi wa wizara amepongeza miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya elimu kwani imekuwa msaada mkubwa kwa miradi ya wizara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: