Gana.. Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).

Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Gana barani Afrika, wameomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).

Majlisi ya kuomboleza imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Markazi inafanya program mfululizo kwenye nchi kadhaa za Afrika, katika kuadhimisha matukio ya Dini na kukumbuka Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Majlisi ya kuomboleza imefanywa katika mji wa Niyu-Abrim nchini Gana chini ya usimamizi wa muwakilishi wa Markazi Shekhe Nasoro Akori”.

Shekhe Akori ameongea kuhusu utukufu wa Imamu Hassan Askariy na nafasi yake kielimu, sambamba na namna alivyo linda umma dhidi ya viongozi waovu wa bani Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: