Atabatu Abbasiyya imetangaza shindano la kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza shindano la kitamaduni katika kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjikuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s), Ataba imeandaa zawadi 20 zinazo fikia dinari za Iraq laki moja (100,000), majina ya washindi yatatangazwa siku ya Jumapili (1/10/2023m) saa kumi jioni, katika jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ili kupata majibu sahihi unatakiwa kusoma vitabu viwili vilivyo andikwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kitabu cha kwanza kinaitwa (Utukufu wa kujivunia katika historia ya Mtume -s.a.w.w-), kitabu cha pili (Imamu Swadiq (a.s) na shule yake kielimu), vitabu hivyo vinapatikana kupitia link ifuatayo:

https://t.me/markazaldirasatalabbas/1574

Ili kushiriki kwenye shindano hili tumia link hii:

https://t.me/markazaldirasatalabbas/1575

Atakaeshinda anatakiwa kufika yeye mwenyewe kupokea zawadi zitakazo tolewa kwenye hafla maalum itakayofanywa mbele ya mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumatatu (tarehe 16 Rabiul-Awwal 1445h) sawa na tarehe (2/10/2023m), iwapo mshindi atakuwa na udhuru wa kufika kwenye hafla hiyo ataenda kupokea zawadi yake kwenye ofisi ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya ndani ya siku tatu (3) toka kutangazwa matokeo, aende na kitambulisho na picha ya rangi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: