Kongamano hilo limeratibiwa na Daaru Rasuulul-A’dham chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, likiwa na kauli mbiu isemayo (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takatifu) na anuani isemayo (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri) kwa muda wa siku mbili, kwenye ukumbi wa Imamu Hassan na Qassim (a.s).
Kikao chu kufunga kongamano kimehuduriwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, mkuu wa Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) Dokta Aadil Nadhiir na viongozi wengi wa kidini na kisekula kutoka ndani na nje ya Iraq.
Kikao kimefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na kusomwa maazimio ya kongamano la awamu ya tatu, yaliyosomwa na Dokta Sha’alani Abdu-Ali.
Hafla ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi wakuu wa vikao vya kongamano, kutoka kwa mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu Dokta Afdhalu Shami, huku rais wa jumuiya ya kielimu ya Al-Ameed akiwakabidhi zawadi watafiti kumi waliowasilisha mada kwenye kongamano hilo, na watafiti wengine wakakabidhiwa zawadi zao na mkuu wa Daaru Rasuulul-A’dham Dokta Aadil Nadhiir.