Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.

Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wapya kwenye mambo tofauti kulingana na fani zao.

Sayyid Rasuul Muhammad Ali kutoka idara ya mahusiano ya ndani chini ya kitengo cha mahusiano amesema “Semina imedumu kwa muda wa siku tano, imejikita katika kuwajengea uwezo watumishi wapya na kubainisha majukumu ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Wamefundishwa mambo ya kitawala, mali, Dini, mahusiano, wametambulishwa vitengo vya Ataba na miradi yake, na mambo mengine mengi yaliyotokana na majadiliano, maswali na majibu”.

Akasema kuwa “Semina ilikuwa na mihadhara ya Akhlaqi na namna ya kuamiliana na watu sambamba na kufundishwa maadili na misingi mizuri katika maadili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: