Majmaa ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inaendelea kupokea mabinti wa Alkafeel.

Kamati zinazosimamia mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq, zinaendelea kufanya maandalizi ya mahafali ya wahitimu hao kwa jina la mabinti wa Alkafeel awamu ya sita, na jengo la Abulfadhil Abbasi (a.s) ni miongoni mwa sehemu itakapofanyika mahafali hiyo.

Mahafali inaandaliwa na kusimamiwa na shule za Alkafeel, itafanywa siku ya Alkhamisi na Ijumaa wiki hii.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Jawadi Hasanawi amesema “Vitengo vyote vitakavyo shiriki vinaendelea kufanya maandalizi na kuhakikisha mahafali inaendana na hadhi ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Leo tunaandalia sehemu za jengo la Abulfadhil Abbasi (a.s) litakalopokea wanafunzi kutoka mikoa tofauti na kuwa mwenyeji wa baadhi ya vipengele vya mahafali hiyo, kwani hapa ndio kituo chao cha kwanza”.

Akasema kuwa maandalizi yanaendelea na yapo katika hatua za mwisho, wamejiandaa kikamilifu kupokea mabinti wa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: