Pembezoni mwa kongamano la kimataifa.. kitengo cha maarifa kinafanya warsha kuhusu jarida la turathi za Karbala na tafiti za kielimu.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya warsha yenye anuani isemayo (Jarida la turathi za Karbala ni msingi wa tafiti za kielimu), muwezeshaji wa warsha hiyo ni mkuu wa wahariri wa jarida Dokta Falahu Alhuseini.

Warsha hii ni sehemu ya kongamano la kielimu liitwalo (Mchango wa Karbala kielimu katika karne ya kumi hijiriyya), linaloratibiwa na kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo na kauli mbiu isemayo (Turathi zetu utaifa wetu), washiriki wanatoka ndani na nje ya Iraq.

Muwezeshaji ameogea kwa ufupi kuhusu uanzishwaji wa jarida hilo na tafiti zinazo andikwa ndani yake.

Akaongea kuhusu anuani ya tafiti na namna ya kufikia malengo ya kielimu na kitafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: