Shada za mauwa zimewekwa juu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi kufuatia kumbukizi ya mazazi ya Aqilatu Zainabu (a.s).

Idara inayosimamia haram takatifu katika Atabatu Abbasiyya, imeweka mauwa kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukizi ya kuzaliwa kwa Aqilatu Zainabu (a.s).

Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twaifu amesema “Watumishi wa idara wamezowea kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), likiwemo hili la kuzaliwa bibi Zainabu (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa vipengele vya kuhuisha tukio hili ni kuweka mauwa mazuri juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu huweka mapambo ya mauwa yenye rangi tofauti juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuadhimisha sikukuu ya Ghadiir na kwenye kumbukizi za kuzaliwa watukufu katika Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: